Jumatano 11 Februari 2026 - 00:04
Wito wa Ayatullah A‘rafi kwa wananchi kushiriki katika matembezi ya tarehe 22 Bahman/ Dunia itaona adhama ya Iran

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran amesema: Kesho itakuwa ni uwanja wa kudhihirika adhama ya Iran na fahari ya taifa, na siku ya ushiriki wa pamoja watu wote katika matembezi ya kihistoria ya tarehe 22 Bahman.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya ujumbe wa wito wa Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu nchini Iran, kwa wananchi ili washiriki kwa hamasa katika matembezi ya kihistoria ya tarehe 22 Bahman ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Katika historia ya mataifa, nyakati nyeti na vipindi maalumu hutokea ambavyo huwa vya kuamua hatima, kuleta mabadiliko, na kuainisha kushuka au kupanda kwa taifa. Kesho, tarehe 22 Bahman 1404, ni miongoni mwa siku za kipekee katika historia ya Iran, Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, na ni katika siku za Mwenyezi Mungu (Ayyamullah). Bila shaka, wananchi wema, vijana wapendwa, pamoja na makundi na tabaka zote za jamii wanatambua kina na upeo wa kimkakati wa sherehe hii na matembezi haya makubwa ya kitaifa na Kiislamu. Wakiwa na kumbukumbu ya mashahidi watukufu na Imam wa mashahidi (r.a), wakifuata uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Mar'aji' wakubwa wa taqlid, na kwa mapenzi ya Uislamu na Iran, wataonesha umoja, mshikamano, nguvu, ujasiri na adhama yao; na Hawza za kielimu, vyuo vikuu na wasomi watakuwa mstari wa mbele wa taifa katika mtihani huu mkubwa.

Kesho itakuwa ni uwanja wa kudhihirika adhama ya Iran na fahari ya taifa, na siku ya uwepo wa pamoja wa watu wote katika matembezi ya kihistoria ya tarehe 22 Bahman. Inatarajiwa kwamba wanazuoni wa dini walio macho na wenye mwamko watatekeleza jukumu lao la kutembea na kuwa mstari wa mbele pamoja na wananchi wapendwa. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa himaya ya Imam wa Zama (a.f), kesho ukurasa wa dhahabu katika kitabu kikubwa cha Mapinduzi ya Kiislamu na Iran pendwa utaandikwa na taifa kubwa na linalostahili kusifiwa la Iran.

Alireza A‘rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha